Hubirini Kwa Sauti
Hubirini Kwa Sauti Lyrics
Hubirini kwa sauti ya kuimba, tangazeni haya
Hubirini kwa sauti ya kinanda, tangazeni haya
Yatamkeni, tamkeni hadi mwisho wa dunia
Semeni Bwana amelikomboa taifa lake
- Mwimbieni Bwana wimbo ule mpya,
Mwimbieni Bwana enyi mataifa
Mwimbieni Bwana kwa sauti ya shangwe,
Mwimbieni Bwana libarikini jina lake
- Tangazeni wokovu siku kwa siku,
Hubirini habari za utukufu
Yahubirini mataifa sifa zake,
Na watu wote habari za ukuu wake
- Mpeni Bwana utukufu na nguvu,
Mpeni Bwana enyi wana wa Mungu
Pelekeni habari zake pande zote,
Mpeni Bwana utukufu wa jina lake
- Mwabuduni Bwana kwa utakatifu,
tetemekeni mbeleze nchi yote
Semeni kwamba Bwana ametamalaki,
Atawahukumu watu wake kwa adili