Matendo ya Mungu

Matendo ya Mungu
Performed bySt. Maria Goretti Karatu Dar-es-Salaam
CategoryInjili na Miito (Gospel)
ComposerBernard Mukasa
Views6,008

Matendo ya Mungu Lyrics

  1. { Nayaleta mbele yenu matendo ya Mungu
    Nayasimulia wazi matendo ya Mungu
    Kwa sauti tamu ni matendo ya Mungu
    Mwendo wa kunesa ni matendo ya Mungu, yasikieni } *2

  2. Farao alipokuwa mgumu,
    Fimbo ya Musa ikawa nyoka hatari, ona
  3. Bahari ikasimama ukuta,
    Naye Israeli akapita pakavu, ona
  4. Kina Shedraki walipochomwa moto
    Wakatembea huku na kule wazima, ona
  5. Jiwe kubwa kaburini kwa Yesu,
    Likampisha akatoka hai kama mwanzo, ona
  6. Nyimbo hizi na midundo ni vyake,
    Asifiwe na ahimidiwe milele, ona