Moto wa Injili
Moto wa Injili | |
---|---|
Performed by | St. Maria Goretti Karatu Dar-es-Salaam |
Category | Injili na Miito (Gospel) |
Composer | E. F. Jissu |
Views | 5,743 |
Moto wa Injili Lyrics
{Moto huu, moto huu wa injili
tuliouwasha tusiuzime bali tuutetee } * 2
{ Haya twende twendeni wote twendeni
Tukaihubiri injili yake Yesu Kristu}- Tusiogope vikwazo wakristu
Hizo ni mbingu za shetani mwovu tusizihofu
Kwani safari ndiyo imeanza
Funga mikanda ndugu usihofu tunaye Mungu - Yapo mataifa yenye njaa
Ya kushibishwa injili ya Yesu ni veyma twende
Na tusipokwenda tuna makosa
Mbele zake Mungu alotuumba tuna hatia - Hata kwa wale wasio na bidii
Tusiwaache wapotee twende tuwape neno
Na tusipokwenda tuna makosa
Mbele zake Mungu alotuumba tuna hatia