Pilka Pilka
Pilka Pilka Lyrics
- Pilka pilka kila siku watu wa dunia
Wanahangaika kutafuta mali za dunia
Asubuhi ni msongamano, mchana vilevile
Usiku shughuli zafanyika kama kawaida
Tafuteni kwanza ufalme ule wa mbinguni
Na hayo mengine (hakika) mtazidishiwa
{Yeye Mungu (Mwenyezi) mtetezi (ajabu)
Mkiamini atawashughilikia } * 2
- Pilika pilika watu wengi kutafuta elimu
Hawakumbuki kwamba Yesu ni mwalimu tosha
Ajali nyingi barabarani zinafanyika kwetu
Tumesahau kwamba Yesu ni dereva tosha
- Pilika pilika twatafuta hospitali kubwa
Huku daktari mkuu ni Mungu wa majeshi
Watu watafuta waganga ili wapate mali
Bali Mungu wa mbinguni ndiye mmliki wa vyote
- Pilika pilika tunawaza usiku na mchana
Vile tutakula vizuri na kuvaa vizuri
Kwani ndege wale wa angani wanalishwa na nani
Kama siyo Mungu wa mbinguni basi huyo nani
- Pilika pilika wenzangu tumuelekee Mungu
Tusifadhaike bali tuwe na matumaini
Atatujalia mema mengi tukiwa duniani
Mwisho tutafurahi na Yesu kule juu mbinguni