Bwana Kama Wewe Ungehesabu Maovu Yetu

Bwana Kama Wewe Ungehesabu Maovu Yetu
Alt TitleNani Angesimama
Performed bySt. Maurus Kurasini
AlbumHubirini Kwa Kuimba
CategoryZaburi
ComposerG. A Chavalla
VideoWatch on YouTube
Views44,666

Bwana Kama Wewe Ungehesabu Maovu Yetu Lyrics

  1. Bwana kama wewe ungehesabu maovu yetu,
    Nani angesimama, nani angesimama
    Nani angesimama mbele yako

  2. Lakini kwako kuna msamaha, ili wewe uogopwe,
    Nimemungoja Bwana, Roho yangu,
    Na neno lake nimelitumaini
  3. Nafsi yangu inamngoja Bwana, kuliko walinzi
    Walinzi waingojavyo asubuhi
    Naam walinzi wangojavyo asubuhi
  4. Ee Bwana toka vilindini, nimekulilia
    Bwana sauti yangu usikie
    Masikio yako yasikie dua zangu
* Pia umerekodiwa na kwaya ya Queen of Apostles Ruaraka * Wimbo huu pia unaweza imbwa wakati wa kwaresma