Hiki ni Chakula kwa Wote
Hiki ni Chakula kwa Wote Lyrics
Hiki ni chakula kwa wote wampendao
Mkate na divai ni chakula cha Roho
Wanyofu wa moyo twendeni tukampokee
Tupate uzima wa milele na milele
- Bwana Yesu alhamisi kuu kajitolea,
Mwili na damu yake ziwe kiburudisho
Akatuamuru tukipenda kumkumbuka,
Mwili na damu ni ishara ya penzi lake
- Alaye mwili na kunywa damu asema Bwana
Aishi ndani yangu na mimi ndani yake
Yeye ni rafiki yangu na nitamfufua,
Nitaandamana naye safarini mwake
- Alaye mwili wa Yesu na kuinywa damu,
Bila stahili ana hukumu ya milele
Tujitakase kabla ya kula karamuyo,
Kitubio ni sakramenti ya mapatano
- Ee Yesu nipe neema ya kukupokea,
Unipe nguvu ya kuweza kujitakasa
Unijalie kukupenda na moyo wote,
Mwishowe nishiriki karamu ya Mbinguni