Nitaimba Siku Zote

Nitaimba Siku Zote
Alt TitleMoyo wa Yesu
Performed byKwaya ya Moyo Safi wa Bikira Maria, Unga Limited Arusha
CategoryMoyo wa Yesu
ComposerJoseph Makoye
Views7,554

Nitaimba Siku Zote Lyrics

  1. { Nitaimba siku zote wa Yesu moyo mkuu
    Kuliko vitu vyote nitapenda moyo huu } *2

  2. Ee moyo mtakatifu wa Yesu Mungu wangu
    Nakuja kukusifu kwa hizi nyimbo zangu
  3. Ee Yesu msalabani kuchomwa ubavuni
    Nitoke utumwani niupate uhuru
  4. Naomba kitu kwako ee Yesu nisikie
    Katika moyo wako ukanijalie
  5. Kwa nini nikapenda furaha za dunia
    Kwa nini sikuenda kwa Yesu kutulia