Ninakushukuru Bwana
Ninakushukuru Bwana Lyrics
- Ninakushukuru Bwana kwa upendo wako
Ninakushukuru Bwana kwa huruma yako
Uliteseka ee Bwana kwa ajili yangu mimi
Ulikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu
(Ni wewe) ni wewe (Bwana)
Ni wewe ni wewe Bwana
(Ni wewe) ni wewe (Bwana)
Ni wewe ni wewe Mwokozi wangu
- Umenijalia Bwana neema zako tele
Ninaishi bila hofu hapa duniani
Kwa kujitolea kwako kwa ajili yangu mimi
Ukapoteza uhai wako unikomboe mimi.
(Ni wewe) ni wewe (Bwana)
Ni wewe ni wewe Bwana
(Ni wewe) ni wewe (Bwana)
Ni wewe ni wewe Mwokozi wangu