Yesu ni Mwema
   
    
     
         
          
            Yesu ni Mwema Lyrics
 
             
            
- Nimetafakari habari zako nami nashindwa kuelewa kabisa
 Binadamu angenipa neema kesho angechoka kunipa zaidi
 Lakini wewe hauna kikomo, wala mvua yako haina majira
 Bwana, wanyesha mvua, Bwana, kwa walio jangwani
 Bwana, wawasha jua, Bwana, mpaka baharini
 Kweli Bwana wewe ni mwema sana
 Nitasimulia miji, Yesu ni mwema, Yesu ni mwema
 Nitahubiri vijini, Yesu ni mwema Yesu ni mwema
 Nitayafafanua haya, Yesu ni mwema Yesu ni mwema
 Watu wote wapate kuyajua, Yesu ni mwema Yesu ni mwema
 Nitasimulia nchi, Yesu ni mwema Yesu ni mwema
- Niliwaza kwa ubinadamu mpaka mwisho wa kufikiri
 Ukataka nijipe moyo, nisihofu kitu
 Kwa kuwa humtupi anayekutumainia
 Ukataka nijipe moyo, nisihofu kitu, kamwe
- Uzoefu wa mapito haya ukaninyima usingizi
 Ukataka nijipe moyo, nisihofu kitu
 Kanuni za dunia zikavunja matumaini
 Ukataka nijipe moyo, nisihofu kitu, kamwe
- Giza lilipotanda mchana likanifunika usoni
 Ukataka nijipe moyo, nisihofu kitu
 Nikapiga kelele hofu kuu ikanisonga
 Ukataka nijipe moyo, nisihofu kitu, kamwe
 
 < h i t i m i s h o>
 
 [t|b] Naimba he he, naimba leo
 Naimba he he, naimba mimi
 Ulijua wazi kwamba mimi sikuwa nastahili,
 Kwa sababu mimi mdhaifu mwili na roho
 Ukaruhusu nifanikiwe juhudi zangu
 Makusudi ili nione ukuu wako
 Ndugu wanipende, jamaa waniheshimu
 Marafiki wanijali, wanisaidie
 Ndiyo maana leo, mimi nakurudishia;
 
 [w] Utukufu ni wako milele
 Sifa heshima ni vyako daima
 Wewe peke yako unastahili
 Usifiwe na uhimidiwe!
 
 Nakushukuru Bwana,  kwa kuwa umeniona asante
 Nakushukuru Bwana,  kwa kuwa umeniona asante
 Nakupa utukufu,  kwa kuwa umeniona asante
 Milele na milele,  kwa kuwa umeniona asante
 Nakushukuru Bwana,  kwa kuwa umeniona asante