Login | Register

Sauti za Kuimba

Yesu ni Mwema Lyrics

YESU NI MWEMA

@ Bernard Mukasa


  Nimetafakari habari zako nami nashindwa kuelewa kabisa
  Binadamu angenipa neema kesho angechoka kunipa zaidi
  Lakini wewe hauna kikomo, wala mvua yako haina majira
  Bwana, wanyesha mvua, Bwana, kwa walio jangwani
  Bwana, wawasha jua, Bwana, mpaka baharini
  Kweli Bwana wewe ni mwema sana

  Nitasimulia miji, Yesu ni mwema, Yesu ni mwema
  Nitahubiri vijini, Yesu ni mwema Yesu ni mwema
  Nitayafafanua haya, Yesu ni mwema Yesu ni mwema
  Watu wote wapate kuyajua, Yesu ni mwema Yesu ni mwema
  Nitasimulia nchi, Yesu ni mwema Yesu ni mwema

  1. Niliwaza kwa ubinadamu mpaka mwisho wa kufikiri
   Ukataka nijipe moyo, nisihofu kitu
   Kwa kuwa humtupi anayekutumainia
   Ukataka nijipe moyo, nisihofu kitu, kamwe
  2. Uzoefu wa mapito haya ukaninyima usingizi
   Ukataka nijipe moyo, nisihofu kitu
   Kanuni za dunia zikavunja matumaini
   Ukataka nijipe moyo, nisihofu kitu, kamwe
  3. Giza lilipotanda mchana likanifunika usoni
   Ukataka nijipe moyo, nisihofu kitu
   Nikapiga kelele hofu kuu ikanisonga
   Ukataka nijipe moyo, nisihofu kitu, kamwe

   < h i t i m i s h o>

   [t|b] Naimba he he, naimba leo
   Naimba he he, naimba mimi
   Ulijua wazi kwamba mimi sikuwa nastahili,
   Kwa sababu mimi mdhaifu mwili na roho
   Ukaruhusu nifanikiwe juhudi zangu
   Makusudi ili nione ukuu wako
   Ndugu wanipende, jamaa waniheshimu
   Marafiki wanijali, wanisaidie
   Ndiyo maana leo, mimi nakurudishia;

   [w] Utukufu ni wako milele
   Sifa heshima ni vyako daima
   Wewe peke yako unastahili
   Usifiwe na uhimidiwe!

   Nakushukuru Bwana, kwa kuwa umeniona asante
   Nakushukuru Bwana, kwa kuwa umeniona asante
   Nakupa utukufu, kwa kuwa umeniona asante
   Milele na milele, kwa kuwa umeniona asante
   Nakushukuru Bwana, kwa kuwa umeniona asante
Yesu ni Mwema
COMPOSERBernard Mukasa
CHOIRSt. Kizito Makuburi
ALBUMNyumba ya Roho
CATEGORYThanksgiving / Shukrani
MUSIC KEYG Major
TIME SIGNATURE6
16
NOTES Open PDF
 • Comments