Mpeni Bwana Utukufu
Mpeni Bwana Utukufu | |
---|---|
Performed by | Maria Mt Mama wa Mungu Musoma |
Category | Zaburi |
Composer | Marcus Mtinga |
Views | 16,651 |
Mpeni Bwana Utukufu Lyrics
{ Mpeni, mpeni Bwana utukufu na nguvu
Mpeni Bwana utukufu na nguvu } *2- Mwimbieni Bwana, mwimbieni Bwana wimbo mpya
Mwimbieni Bwana, nchi yote,
Wahubirini mataifa habari za utukufu wake
Na watu wote habari za maajabu yake - Kwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kusifiwa sana
na wa kuhofiwa kuliko miungu yote
Maana miungu yote si kitu
Lakini Bwana ndiye aliyezifanya mbingu - Mpeni Bwana mpeni Bwana enyi jamaa za watu
mpeni utukufu wa jina lake
Leteni sadaka mkaziinua
Na tetemekeeni mbele zake
Semeni Mungu ndiye mfalme