Imani Yangu
Imani Yangu | |
---|---|
Performed by | St. Maria Goretti Karatu Dar-es-Salaam |
Category | Faith |
Composer | Victor Aloyce Murishiwa |
Views | 7,667 |
Imani Yangu Lyrics
IMANI YANGU
Niko katikati ya mbingu na ardhi,
Ninaning'inia sina pa kushika
Duniani sipo na mbinguni sipo
Ninawayawaya Bwana niokoe
/s/ Nikienda huku mambo moto moto
Nikienda kule ni baridi tupu
Mbele yangu giza, nyumba yangu giza
Mahubiri mengi yananiyumbisha imani
/a/ kumtafuta Mwokozi
Ee Mungu wangu uko wapi, ili nije kwako hima,
Mbele yangu kuna giza nene, na nyuma yangu
ni giza, mahubiri mengi yamezidi
Na mengine yananiyumbisha imani
/t/ Nikienda huku ninabatizwa na
nikirudi (kule) ninaitwa mimi kafiri
Giza pande zote mahubiri ni mengi
Na mengine yananiyumbisha imani
/b/ nikienda huku ni moto nikirudi huku baridi
Vuguvugu haitakiwi na imani yangu yayumba
Mungu wangu nisaidie niokoe nisipotee
Mahubiri mengi
Na mengine yananiyumbisha imani- Manabii wengi wananiyumbisha,
Nifuate yupi nimuache yupi
Wapo wa uongo, wapo wa kweli,
Njoo Bwana Yesu Rudi kwetu hima
Ulimwengu huu ulioufia umekuwa Jela la maskini - Roho yangu Bwana inakutamani
wewe peke yako ndiwe tiba yangu
neno lako Bwana litaniponya
Kwa sababu wewe Mungu ni mmoja
Twakuomba Baba utuunganishe
Matabaka yote na yatoweke