Ni Mungu Mkuu
Ni Mungu Mkuu Lyrics
- Ni Mungu mkuu *3 ni Mungu wa ushindi
Ni Mungu mkuu *3 ni Mungu wa uweza
Ni Mungu mkuu *3 ni Mungu wa ushindi
Ni Mungu mkuu uuu mkuu
Ni Mungu mkuu ni Mungu wa ushindi
Ni Mungu wa uweza
- Ameumba jua na mwezi,
vinavyong'ara vyote kaumba
Ameumba radi inayonguruma,
yenye kutisha yenye kuogofya
- Ameumba giza na kimya
akaviumba vilivyo tuli
Ameumba maji yanayofariji,
yenye kupoza na kuburudisha
- Astahili sifa na utukufu,
Astahili enzi na utawala
Astahili kusifiwa na kutukuzwa,
Astahili kusifiwa milele milele
- Astahili sifa, astahili enzi *2
Astahili sifa, Astahili sifa na heshima
Astahili sifa *2 sifa astahilina heshima
- Kaweka mamlaka zake mikononi mwa watu
Ni watu wadogo mno kwenye koo duni tu
Kawapa fimbo yake kuu wamchungie kondoo
Wakaifanye kazi kwenye shamba lake kuu
- Ndiye Mungu wa babu abrahamu na wa Isaka
(Na yeye) Ndiye Mungu wa Yakobo na daudi
Ni Mungu wa milele
- Ni Mungu mkuu * 2 ni Mungu wa ushindi
Ni Mungu mkuu *2 ni Mungu wa uweza
- {Astahili kusifiwa kutukuzwa milele *2
Ni Mungu mkuu wa ushindi,
Ni Mungu mkuu wa uweza
Ni Mungu Mungu hutenda makuu } * 2
- Ni Mungu mkuu *3 ni Mungu wa ushindi
Ni Mungu mkuu *3 ni Bwana wa mabwana