Mwalimu Mwalimu Tazama

Mwalimu Mwalimu Tazama
Performed bySt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumMbinguni Kutakuwa Raha (Vol 4)
CategoryMafundisho ya Yesu
ComposerJ. C. Shomaly
Views6,048

Mwalimu Mwalimu Tazama Lyrics

  1. Mwalimu mwalimu hebu tazama tazama tazama
    Jinsi mawe haya na majengo haya yalivyo mazuri

    [b] Naye mwalimu akasema -
    [w] {Hakuna hata kimoja kitakachosalia (humu)
    Tarumbeta yake Bwana itakapolia,
    (vyote) Vitabomolewa vitabomolewa, siku hiyo inakuja} *2

  2. Kesheni kesheni msije ingia majaribuni
    Kesheni kesheni Bwana asiwakute mmelala.
  3. Zitubuni dhambi kwa unyenyekevu ili muokoke
    Kemeeni anasa pia nayo matendo machafu.
  4. Saidieni maskini pia na wote wajane
    Msipende kulipwa kwa yale yote mnayoyatenda