Bado Nahitaji Kufanya Bidii

Bado Nahitaji Kufanya Bidii
Alt TitleBado Nahitaji
Performed bySt. Theresa wa Mtoto Yesu, Mwanza
CategoryTafakari
ComposerE. Nyanza
Views7,041

Bado Nahitaji Kufanya Bidii Lyrics

  1. { Bado nahitaji (nahitaji) kufanya bidii
    Bado nahitaji kufanya bidii kwa kuwa } *2
    sina cha kujivunia mbele za Bwana
    { Nikitazama matendo yangu na mawazo yangu
    Si kitu mbele za Bwana hata anitazame } *2

  2. Nayatolea maisha yangu kuleta amani
    Maelewano palipo na utengano
  3. Uniwezeshe ee Mungu wangu niwalete kwako
    Wale ambao bado hawajakujua
  4. Hata nikifanya hivyo bado, sioni lolote
    Niongoze nifanye mapenzi yako