Nyamazeni Sasa Lyrics

NYAMAZENI SASA

@ Bernard Mukasa

{He he! he he! Nyamazeni sasa mkae kimya,
(nyamazeni) nyamazeni sasa mkae kimya! }*2
Nendeni mkajifunze upendo nenda
(nenda ndugu) Kapunguzeni maneno mengi
(mengi tena) Acheni ufarisayo kando
(kando Kisha) Mkajifunze upendo nenda

 1. Kulitajataja jina la Yesu, na kutolitaja taja kabisa
  Yote ni sawa kabisa mmmh mmh
  Lililo la muhimu, upendo,
  Kuvumilia yote, upendo
  Kuamini yote, upendo,
  Kutumaini yote, upendo
 2. Kusudi watu wasiwatambue kwa yale mnayosema
  Kwa yale maneno, bali kwa matendo tu
  Kwa kuwathamini na kuwajali wenzenu daima *2
  Kwa kuwakumbuka wale walio wadogo na wanyonge
  Kwa kuwakumbuka wale walio wadogo na!
  he! he! upendo! *3 he! upendo
Nyamazeni Sasa
COMPOSERBernard Mukasa
CHOIRSt. Kizito Makuburi
ALBUMNyumba ya Roho
CATEGORYTafakari
MUSIC KEYE Major
TIME SIGNATURE6
16
NOTES Open PDF
 • Comments