Ramani ya Mbinguni
Ramani ya Mbinguni Lyrics
Naisafisha njia (mimi) - njia iendayo Mbinguni *2
Nilikoahidiwa (mimi) - makao ya milele mimi
Naisafisha njia - njia iendayo Mbinguni
Tena - Sina wasiwasi, wala - hofu ndani ya moyo
Kwa kuwa - ninayo ramani, ramani ya mbinguni
Tena - ninapoisoma, hii ramani ya mbinguni
Nakiri - nitauona, upendo wa Mungu kwangu
- Asante Bwana Mungu - (aee) aee (aee) aee (aee)
Kwa kunipenda mimi - ae ee aeee aee
Ukanipa ramani - (aee) aee (aee) aee (aee)
Ramani iniongoze inifikishe uliko ee Mungu wangu.
- Asante Bwana Yesu -
Kwa kunipenda mimi -
Ukaja duniani -
Ili tu unikomboe unitoe utumwani mwake shetani
- Asante Roho mtakatifu -
Kwa kunipenda mimi -
Kwani huniongoza
Katika hii safari kuelekea mbinguni kwa Mungu Baba