Tanzania
   
    
     
         
          
            Tanzania Lyrics
 
             
            
- Mwenyezi Mungu Rahimu na mradhi mwema,
 salamu salamu Mwumba wa Adamu
 Watanzania tumekuja kwa wimbo,
 na tenzi kuongea nawe leo hii
 Uchaguzi mkuu huu tunaoandaa,
 twaomba ujae baraka zako kuu
 Kusudi uwepo wako udhihirike,
 katika serikali tutakayounda
- Rais mpya awe fimbo bora,
 awe taa ya kweli kwenye kinara
 Wabunge wawe matawi mazuri,
 yenye kuzaa kwenye mti wa rutuba
 Madiwani wawe watu wa watu,
 kuongoza watu kwa ajili ya watu
 Tujenge Tanzania madhubuti,
 mioyoni badala ya ardhini
- Wagonjwa wapone, makiwa wafarijiwe,
 masikini waonje maziwa kila siku
 Wajane waishi, yatima waende shule,
 fukara waone thamani ya utu wao
 Majanga yakome, majeruhi watibiwe,
 walio gerezani wawe huru mitaani
 Undugu ukue, amani iongezeke,
 na wahalifu wote wabadilishe tabia
- Na watoto, watoto wadogo,
 walelewe kwa maadili
 Madhehebu, yote ya kidini,
 yawe tahadhari ya upendo
 Navyo vyama, vyetu vya siasa,
 viwe siri kuu ya amani
 Ibilisi, afunge virago,
 aondoke kamwe asirudi!
- Kiapo atakachoapa rais mpya,
 kidumu hata hatimamu ya dahari
 Majaribu yote yatakayotukumbuka,
 yapimwe yasizidi kimo chetu
 Mwenyezi Mungu rahimu twakuomba,
 tulinde tulinde bila ya kuchoka
 Ili mwisho wa safari ya hapa,
 tufike mbinguni wote Tanzania