Tazama Mimi
Tazama Mimi | |
---|---|
Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
Category | Mafundisho ya Yesu |
Composer | J. C. Shomaly |
Views | 5,065 |
Tazama Mimi Lyrics
- Tazama mimi mwanitafuta ni kwa sababu mlikula mikate
Na wala si kwa sababu ninyi mliona zile isharaNa mimi ee Bwana nakutafuta kwa moyo wote
Nione ishara nayo matendo nifike kwako
{ Najilaza chini, kifudifudi,
Ningali kijana unibariki na kizazi changu }* 2 - Tazama mimi nilitumwa ili niuokoe ulimwengu
Na wala si kwa sababu nijiinue ili muamini - Tazama mimi sikuja kuwaita wema bali wenye dhambi
Na wala sikuja ili yao watu wema wajinyanyue - Tazama mimi niko pamoja nanyi siku zote niko nanyi
Siku zote siku zote hata ukamilifu wa dahari