Siri ya Mafanikio
| Siri ya Mafanikio | |
|---|---|
| Performed by | BMT Ledochowska K/Ndege Dodoma | 
| Album | Dawa ya Uzima | 
| Category | Tafakari | 
| Views | 4,951 | 
Siri ya Mafanikio Lyrics
- Nikateleza nikatapatapa,
 sauti ile ikanirudia tena
 Ikanambia usiwe na hofu,
 inua macho yako kwenye mti huu (na kisha)Tazama tundu hili takatifu la neema
 Kwenye moyo uliojaa pendo
 Na ndilo siri ya mafanikio ya maisha
 Ya furaha na amani ya kweli (aleluya)
 Wa Yesu umefunuliwa moyo huo
 Nauona uko wazi moyo ( tukufu)
 Unanimiminia neema moyo huo
 Uko wazi uko wazi moyo
- Ulipochomwa kwa chuma kigumu,
 na ni ugumu ule wa mioyo yetu
 Ukatujibu kwa kumwaga maji,
 maji laini nayo damu ya sadaka (lakini)
- Hauchukii hauna kisasi,
 moyo mpole mwema na mnyenyekevu
 Shida na tabu tukiukabidhi,
 unachotoa ni neema na ushindi
- Mahangaiko na kumaka kwetu,
 tuupelekee moyo wake Yesu
 Tutafurahi tutafanikiwa,
 damu na maji yake yatatutakasa (lakini)
- Ili daima atukuzwe Baba,
 na mwana atukuzwe Roho Mtakatifu
 Ilivyokuwa toka kule mwanzo,
 sasa na siku zote daima milele (amina)
 
  
         
                            