Toa Kwanza Boriti

Toa Kwanza Boriti
Performed bySt. Bernardette Kisii
CategoryMafundisho ya Yesu
Views9,544

Toa Kwanza Boriti Lyrics

  1. Toa kwanza boriti ndani ya jicho lako
    Ndipo uone kibanzi ndani ya jicho la ndugu yako
    {Maana utamwambiaje, utamwambiaje nduguyo
    Hebu nikitoe kibanzi, ndani ndani ya jicho lako
    (Na kumbe mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe) *2}

  2. Msihukumu msije mkahukumiwa nyinyi
    Hukumu mhukumuyo ndiyo mtahukumiwa nyinyi
    Kipimo mpimiacho ndicho mtakachopimiwa
  3. Ombeni nanyi mtapewa/ tafuteni nanyi mtaona/
    Bisheni nanyi mtafunguliwa

    Basi yoyote myatakayo mtendewe na watu/
    nanyi watendeeni vivyo hivyo
    Maana hiyo ndiyo torati ya manabii