Ukiwaona Kama Watu

Ukiwaona Kama Watu
Performed bySt. Don Bosco Mirerani
AlbumRamani ya Mbinguni
CategoryTafakari
ComposerE. F. Jissu
Views6,444

Ukiwaona Kama Watu Lyrics

  1. Ukiwaona kama watu - hao, kama watu
    Kumbe ndani ni mbwa mwitu - hao, mbwa mwitu
    Wamejivika mavazi ya kondoo * 4

  2. Sura zao zinavutia machoni pa watu
    Na kuonekana wao ni wa maana kwa watu
    Matapeli wakuu ni wao, ni wao, ni wao wanadamu
    Wala rushwa wakuu ni wao, ni wao, ni wao wanadamu
  3. Vinywa vyao hunena maneno matamu kwa watu
    Na kuonekana wenye hekima nyingi kwa watu
    Kumbe ndani hao ni wachafu (wachafu *2) wanadamu
    Wanadhani Mungu hawaoni (wachafu *3) wanadamu
  4. Kwa ushirikina wao ni viongozi hodari
    Hujisifia kwa mambo yao maovu kwa watu
    Kumbe wanajilisha upepo mchafu
    Kwa hivyo unayo hii (nafasi *2) kwa Mungu mwanadamu
  5. Ufisadi uso na mfano ni wao ni wao
    Ukiwaona wala huwezi dhania ni wao
    Kweli ndugu inasikitisha, ni wao, ni wao wanadamu
    Hawamuogopi hata Mungu ni wao ni wao wanadamu
  6. Nyumba za ibada hawakosekani, kwa kweli
    Na nyadhifa pia wanajitwalia aibu
    Mnamdhalilisha Mungu, Mungu, Mungu, wanadamu
    Elewa Mungu anakuona, kuona, kuona, mwanadamu