Jawabu la Moyo Wangu

Jawabu la Moyo Wangu
Performed bySt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumUshuhuda Tosha
CategoryThanksgiving / Shukrani
ComposerJ. C. Shomaly
Views4,454

Jawabu la Moyo Wangu Lyrics

  1. Usione ninaimba nafurahia naburudika
    Maisha yangu mazuri, amani tele moyoni mwangu
    (Ni Mungu) anipaye nguvu, (ni Mungu) anipaye afya
    (Ni Mungu) ananiongoza, (ni Mungu) msaada wangu
    Jawabu langu la moyo wangu ndiye Mungu,
    Mungu Baba anilindaye anilindaye mimi

  2. Jawabu la moyo wangu ni Mungu shahidi yangu
    Nikiwa na matatizo anijalia faraja
  3. Nimezungukazunguka, maisha yangu hafifu
    Nikamrudia Mungu, sasa ninatabasamu
  4. Njia zake ndizo njia, mapendo yake makuu
    Kanipa heshima kubwa, mbele ya adui zangu