Login | Register

Sauti za Kuimba

Jawabu la Moyo Wangu Lyrics

JAWABU LA MOYO WANGU

@ J. C. Shomaly

Usione ninaimba nafurahia naburudika
Maisha yangu mazuri, amani tele moyoni mwangu
(Ni Mungu) anipaye nguvu, (ni Mungu) anipaye afya
(Ni Mungu) ananiongoza, (ni Mungu) msaada wangu
Jawabu langu la moyo wangu ndiye Mungu,
Mungu Baba anilindaye anilindaye mimi

  1. Jawabu la moyo wangu ni Mungu shahidi yangu
    Nikiwa na matatizo anijalia faraja
  2. Nimezungukazunguka, maisha yangu hafifu
    Nikamrudia Mungu, sasa ninatabasamu
  3. Njia zake ndizo njia, mapendo yake makuu
    Kanipa heshima kubwa, mbele ya adui zangu
Jawabu la Moyo Wangu
COMPOSERJ. C. Shomaly
CHOIRSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
ALBUMUshuhuda Tosha
CATEGORYThanksgiving / Shukrani
  • Comments