Duka la Shetani
Duka la Shetani | |
---|---|
Alt Title | Usipange Foleni |
Performed by | St. Veronica Kariakor Dar-es-salaam |
Album | Kama Nyuki |
Category | Tafakari |
Composer | Victor Aloyce Murishiwa |
Views | 6,387 |
Duka la Shetani Lyrics
Usipange foleni kwenye duka la shetani
Utauziwa dhambi faida yake mauti
Nenda ukajipange dukani kwa Bwana Yesu
Utapata kibali cha kuingia mbinguni- Enyi wavuta bangi, na madawa ya kulevya
Mbona mmejipanga katika duka la shetani - Na ninyi wala rushwa, makahaba na wachawi
Mbona mmejipanga katika duka la shetani - Duka lake shetani limejaa vitu vingi
Tena vyapendeza sana na kuuvutia moyo - Ramani ya mbinguni nenda kwake Yesu
Ramani ya kuzimu shetani ndiye mchoraji - Mnaofunga ndoa katika jinsia moja
Nanyi mmejipanga katika duka la shetani - Mavazi ya aibu dada zetu mwajivika
Mnaita vimini shetani anachekelea