Yesu Kanikuta Jangwani

Yesu Kanikuta Jangwani
ChoirOur Lady of Guadalupe
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
Composer(traditional)
SourceTanzania

Yesu Kanikuta Jangwani Lyrics

 1. Yesu kanikuta jangwani, akaniambia, nenda huko Yerusaleme
  Yesu kanikuta gizani, akasema, kimbilia Yerusaleme

  Mimi ni kipofu ni mauti (mimi ni mauti)
  Mimi ni kipofu sioni (mimi sioni)
  { Kulikuwa giza, kukapambazuka
  Nikamwona Bwana Bwana wangu }*2

 2. Natamani mji ule, Yerusaleme kuna nuru kuna raha
  Dhambi zangu matendo yangu, ni maovu, tazameni msalabani

  Upindo wa nguo (nguo yako safi)
  Upindo wa nguo (nguo yako nzuri)
  { Uniguse moyo, moyoni mwangu
  Nitaimba sifa sifa zako } *2

 3. Watakatifu wa moyo, tumsifuni, Bwana mwenye nchi na mbingu
  Twende huko nchi ya mbali, ya Kanaani ndiko tutaishi milele

  { Fimbo yake Musa ilituokoa
  Fimbo yake Musa, ilituongoza
  { Nchi ile ya Misri (nchi ya farao)
  Tulimwona Bwana mwenye enzi } }*2