Enyi Wanadamu
| Enyi Wanadamu |
|---|
| Performed by | - |
| Category | Tafakari |
| Composer | J. C. Shomaly |
| Views | 4,027 |
Enyi Wanadamu Lyrics
Enyi wanadamu msisumbukie maisha yenu
Kwani yale yote mnayoyasumbukia Mungu anayajua
{ Msijiulize ulize kwamba mtaishi vipi
Bali utafuteni kwanza ufalme (wa Mungu)
Nayo mahitaji yenu mnayohangaikia
kila siku Mungu atawapa } *2
- Msifikiri sana, juu ya maisha yenu
Bali mtumikieni Mungu,
Kwa kusali na kutenda mema,
Kwa kuwa Mungu ndiye mtoaji wa vyote
- Jueni Mungu ndiye, kinga ya maisha yenu
Sasa mtumikieni Mungu,
Kwa kusali na kutenda mema,
Kwa kuwa Mungu ndiye mtoaji wa vyote