Login | Register

Sauti za Kuimba

Enyi Wanadamu Lyrics

ENYI WANADAMU

@ J. C. Shomaly

Enyi wanadamu msisumbukie maisha yenu
Kwani yale yote mnayoyasumbukia Mungu anayajua
{ Msijiulize ulize kwamba mtaishi vipi
Bali utafuteni kwanza ufalme (wa Mungu)
Nayo mahitaji yenu mnayohangaikia
kila siku Mungu atawapa } *2

 1. Msifikiri sana, juu ya maisha yenu
  Bali mtumikieni Mungu,
  Kwa kusali na kutenda mema,
  Kwa kuwa Mungu ndiye mtoaji wa vyote
 2. Jueni Mungu ndiye, kinga ya maisha yenu
  Sasa mtumikieni Mungu,
  Kwa kusali na kutenda mema,
  Kwa kuwa Mungu ndiye mtoaji wa vyote
Enyi Wanadamu
COMPOSERJ. C. Shomaly
CATEGORYTafakari
REFLk. 12; Mt. 6
SOURCESt. Paul's Chapel University of Nairobi Students Choir
 • Comments