Naitazama Imani Yangu

Naitazama Imani Yangu
Performed bySt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumUshuhuda Tosha
CategoryFaith
ComposerJ. C. Shomaly
Views4,324

Naitazama Imani Yangu Lyrics

  1. Natazama upande upande nikisema haya,
    Siyo kwamba mimi naogopa maadui zangu
    Nataka wote wayasikie wamwamini Mungu

    { Naitazama imani yangu isiyumbeyumbe (kabisa) Nayatazama matendo yangu yasirudi nyuma (ah)
    Upendo wako ni raha yangu ndani ya roho
    Kikombe kile chake shetani mimi nisikinywe
    Kabisa aaa ah kabisa 1(ni mimi ninasema) } *2

  2. Umenitoa mbali ee Mungu siwezi kusema,
    Wengi waliniita mgumba sasa nanyonyesha
    Nataka wote wayasikie wamwamini Mungu
  3. Waliponidharau mnyonge mimi sina mali,
    Leo umenibariki mimi ninaishi vema,
    Nataka wote wayasikie wamwamini Mungu
  4. Kazi zangu nilizozifanya walizidharau
    Kupitia kwa mkono wako umeniinua
    Nataka wote wayasikie wamwamini Mungu
  5. Shukurani yangu ninatoa kwako Mungu wangu
    Sina cha kulipa mema mengi ulotenda kwangu
    Nataka wote wayasikie wamwamini Mungu