Milele Milele Msifuni
   
    
     
         
          
            Milele Milele Msifuni Lyrics
 
             
            
- Milele milele msifuni Bwana
 Na ahimidiwe Bwana milele,
 Amina, amina, aleluya
 Rehema za Bwana ni za milele
 Na uaminifu wa Mungu wetu,
 Ni kwa vizazi hata vizazi
 { Njooni, tuimbe, tumwimbie Bwana
 Yeye (ndiye) wokovu, wokovu wetu (Bwana)
 Ni Mungu wetu na mwumba wetu, aleluya aleluya } *2
- Nitakushukuru ee Bwana Mungu
 Nitalishukuru jina la Bwana,
 Ee Bwana mfalme Mungu wangu
 Pigeni vigelegele pigeni
 Pigeni magoti mbele za Bwana
 Kwa maana ndiye Mungu wetu
- Atawabariki wamchao Bwana
 Wadogo wakubwa awabariki
 Msaada wao na ngome yao
 Tazama atabarikiwa hivyo
 Atabarikiwa amchaye Bwana
 Awabariki toka Sayuni