Milele Milele Msifuni

Milele Milele Msifuni
ChoirManzese
CategoryThanksgiving / Shukrani
ComposerM. B. Syote

Milele Milele Msifuni Lyrics

 1. Milele milele msifuni Bwana
  Na ahimidiwe Bwana milele,
  Amina, amina, aleluya
  Rehema za Bwana ni za milele
  Na uaminifu wa Mungu wetu,
  Ni kwa vizazi hata vizazi

  { Njooni, tuimbe, tumwimbie Bwana
  Yeye (ndiye) wokovu, wokovu wetu (Bwana)
  Ni Mungu wetu na mwumba wetu, aleluya aleluya } *2

 2. Nitakushukuru ee Bwana Mungu
  Nitalishukuru jina la Bwana,
  Ee Bwana mfalme Mungu wangu
  Pigeni vigelegele pigeni
  Pigeni magoti mbele za Bwana
  Kwa maana ndiye Mungu wetu
 3. Atawabariki wamchao Bwana
  Wadogo wakubwa awabariki
  Msaada wao na ngome yao
  Tazama atabarikiwa hivyo
  Atabarikiwa amchaye Bwana
  Awabariki toka Sayuni