Mkumbuke Mungu Lyrics

MKUMBUKE MUNGU

@ J. C. Shomaly

{ Mkumbuke Mungu wakati wa ujana wako
Siku zisije pita, mpaka wakati wa uzee wako } *2

 1. Kama wewe ni msichana
  Mara hiyo hiyo mkumbuke Mungu
  Na usingoje uchakae
  Mara hiyo hiyo mkumbuke Mungu
  Kama wewe bado kijana
  Mara hiyo hiyo mkumbuke Mungu
  Na usingoje uzeeke
  Mara hiyo hiyo mkumbuke Mungu
 2. Kama wewe ni kiongozi . . .
  Na usingoje ustaafu . . .
  Kama wewe ni daktari . . .
  Na usingoje utibiwe . . .
 3. Biashara ikikubali . . .
  Na usingoje ikatae . . .
  Na masomo yakikubali . . .
  Na usingoje uwe zuzu . . .
 4. Ukiwa na nguvu kijana . . .
  Na usingoje ulemae . . .
  Ukiwa na gari kijana . . .
  Na usingoje uishiwe . . .
Mkumbuke Mungu
COMPOSERJ. C. Shomaly
CHOIRSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
ALBUMUshuhuda Tosha
CATEGORYTafakari
 • Comments