Shukrani Yangu
| Shukrani Yangu | |
|---|---|
| Alt Title | Hii Sio Hadithi | 
| Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) | 
| Album | Ushuhuda Tosha | 
| Category | Thanksgiving / Shukrani | 
| Composer | J. C. Shomaly | 
| Views | 7,737 | 
Shukrani Yangu Lyrics
- Hii sio hadithi ninataka kusimulia
 Wala sio historia wala si somo la siasa
 Ni mambo mema sana aliyotenda Mungu kwangu
 Na nisipoyatamka nitakuwa sina fadhilaWazazi wamenilea mpaka nimefika hapa
 Majirani na ndugu zangu pia wamenipiga jeki
 [ b ] Baba usikie sala hii mimi natoa
 { Wabariki wazazi wangu wape maisha marefu
 Wabariki na ndugu zangu wape amani tele
 Marafiki zangu pia mimi mwenyewe
 Siwezi kusahau kuwaombea na adui zangu } *2
- Mungu ninakushukuru, afya njema wanijalia
 Kila ninapoamka sijui nitakupa nini
 Masomo yangu nasoma pia ninafaulu vyema
 Sasa nimefika hapa sio kwamba mimi ni mwema
- Shuleni niliposoma nilikuwa na marafiki
 Waliosoma vizuri pia na wenye afya njema
 Sio wote waliweza kufikia nilipofika
 Nashindwa niseme nini jinsi umenipenda mimi
- Vijijini nimeishi watu wengi nimewaona
 Hawana mbele na nyuma wameishia kunywa pombe
 Maisha yao magumu elimu yao haba haba
 Nashindwa nikupe nini hapa nilipofika mimi
- Siwezi kusema mengi najua wewe ndiwe kinga
 Nibariki nijalie maisha yenye kupendeza
 Kipaji nilicho nacho cha kuimba na kuhubiri
 Kiwavute watu wengi wakuabudu wewe Bwana
 
  
         
                            