Siku Ile Niliyokuita
Siku Ile Niliyokuita | |
---|---|
Performed by | Kwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha |
Category | Zaburi |
Composer | J. D. Mkomagu |
Views | 4,883 |
Siku Ile Niliyokuita Lyrics
{ Siku ile niliyokuita, uliniitikia,
Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu
Nitashukuru kwa moyo wangu (moyo) wote
Mbele ya miu-ngu nitakui-mbia zaburi
(Nami ) nitakusujudu nikilikabili
Hekalu lako takatifu, hekalu lako takatifu } *2- Nitalishukuru jina lako, kwa ajili ya fadhili zako
Na uaminifu wako, kwa maana umeikuza
Ahadi yako kuliko jina lako lote - Ingawa Bwana yuko juu, amuona mnyenyekevu
Naye amjua mwenye kujivuna tokea mbali
Nijapokwenda katika shida utanihuisha
Utanyoosha mkono juu ya hasira za adui