Ushuhuda Tosha
Ushuhuda Tosha | |
---|---|
Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
Album | Ushuhuda Tosha |
Category | Thanksgiving / Shukrani |
Composer | J. C. Shomaly |
Views | 6,253 |
Ushuhuda Tosha Lyrics
- Tuna haki ya kutamka na kutoa ushuhuda
Mambo mema alotenda Mungu pia na kwa huruma
Ninamwambia naye jirani Mungu ana huruma{ Ushuhuda, huo ni ushuhuda tosha (nasema)
Ni huruma, Mungu ana huruma nyingi (hakika)
Ninapolala pia ninaamka huo wote ni ushuhuda tosha } *2 - Kaumba mbingu na dunia wanyama hata samaki
Binadamu na akili nyingi sisi tukawatawale
Kwa kweli Mungu ana huruma kwetu binadamu - Tunalala bila kuomba hatimaye twaamka
Mungu wetu na hakasiriki bado atupa mkate
Kwa kweli Mungu ana huruma kwetu binadamu - Maisha yetu twayapanga nayo yanafanikiwa
Mara nyingi hata hatuombi kumshirikisha Mungu
Kwa kweli Mungu ana huruma kwetu binadamu - Tunapofanya biashara uongo tunatumia
Twazikiuka amri za Mungu ili tupate faida
Kwa kweli Mungu ana huruma kwetu binadamu - Ni mengi hatujatamka wanadamu tunafanya
Tunaomba msamaha Mungu sisi sote walegevu
Kwa kweli Mungu ana huruma kwetu binadamu