Login | Register

Sauti za Kuimba

Ushuhuda Tosha Lyrics

USHUHUDA TOSHA

@ J. C. Shomaly

 1. Tuna haki ya kutamka na kutoa ushuhuda
  Mambo mema alotenda Mungu pia na kwa huruma
  Ninamwambia naye jirani Mungu ana huruma

  { Ushuhuda, huo ni ushuhuda tosha (nasema)
  Ni huruma, Mungu ana huruma nyingi (hakika)
  Ninapolala pia ninaamka huo wote ni ushuhuda tosha } *2

 2. Kaumba mbingu na dunia wanyama hata samaki
  Binadamu na akili nyingi sisi tukawatawale
  Kwa kweli Mungu ana huruma kwetu binadamu
 3. Tunalala bila kuomba hatimaye twaamka
  Mungu wetu na hakasiriki bado atupa mkate
  Kwa kweli Mungu ana huruma kwetu binadamu
 4. Maisha yetu twayapanga nayo yanafanikiwa
  Mara nyingi hata hatuombi kumshirikisha Mungu
  Kwa kweli Mungu ana huruma kwetu binadamu
 5. Tunapofanya biashara uongo tunatumia
  Twazikiuka amri za Mungu ili tupate faida
  Kwa kweli Mungu ana huruma kwetu binadamu
 6. Ni mengi hatujatamka wanadamu tunafanya
  Tunaomba msamaha Mungu sisi sote walegevu
  Kwa kweli Mungu ana huruma kwetu binadamu
Ushuhuda Tosha
COMPOSERJ. C. Shomaly
CHOIRSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
ALBUMUshuhuda Tosha
CATEGORYThanksgiving / Shukrani
 • Comments