Nikitazama Chini ya Jua
Nikitazama Chini ya Jua | |
---|---|
Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
Album | Ushuhuda Tosha |
Category | Thanksgiving / Shukrani |
Composer | J. C. Shomaly |
Views | 4,047 |
Nikitazama Chini ya Jua Lyrics
{ Nikitazama chini ya jua hili ulofanya Mungu,
Utukufu ni wako na sifa unastahili Mungu } * 2
{ Asubuhi na jioni, mchana hata usiku
Watu kazi mbalimbali, riziki ni tofauti
Vyote umevifanya utukufu sifa ni zako Mungu} * 2- Majira na nyakati, kiangazi mvua hata na masika
Vyote umevifanya utukufu sifa ni zako Mungu - Binadamu twaishi yote haya mpango wako ee Mungu
Vyote umevifanya utukufu sifa ni zako Mungu