Jeshi la Malaika
Jeshi la Malaika | |
---|---|
Alt Title | Jina Kuu |
Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
Album | Ushuhuda Tosha |
Category | Tafakari |
Composer | J. C. Shomaly |
Views | 5,006 |
Jeshi la Malaika Lyrics
- Sasa jeshi la malaika lashangilia jina hili tukufu
Na sisi viumbe duniani twashuhudia utukufu mkuu
Twaungana na malaika tukisifu sana jina hili ni kuu
Tangu Yohane atabiri na sisi sote hatuliasi ni kuuTwimbe twimbe tumsifuni Yesu, jina lake latenda makuu
Mfalme Kristu mwana wake Mungu
Tumsifuni tumsifuni tumshukuru Mungu - Dhambi yake Adamu babu na bibi Eva ilikuwa asili,
Mkombozi Yesu katumwa dunia yote sisi kutuokoa
Waliokuwa na kiburi ni ibilisi na wenye shingo ngumu
Wamebaki midomo wazi wakiteketea kwa moto mkali - Wasioamini na wasiomkubali kwao ni kama ndoto,
Muda wao ukishapita kilio chao mavuno ni mkaa
Mawazo yao duni sana na mbinu zao zisizoenda mbali,
Wasiokubali ya kuwa Mungu ndiye mweza wa kila kitu - Kina Baba mama vijana pia watoto jueni hili jambo
Dunia yote ina mwisho ya duniani ni ya muda mfupi
Biashara zisiwe nyingi mkasahau aliyetuumba sisi,
Mwenye uwezo wa kutoa pumzi na afya yapaswa tumtii