Upendo Kupita Upeo

Upendo Kupita Upeo
Alt TitleEe Mungu Wangu
Performed bySt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumUshuhuda Tosha
CategoryThanksgiving / Shukrani
ComposerJ. C. Shomaly
Views6,691

Upendo Kupita Upeo Lyrics

  1. Ee Mungu wangu, kwa hakika unanipenda
    Upeo wa macho yangu, sijui nikulipe nini
    Maisha yangu, nayatazama nashukuru
    Kwa yote uliyotenda, na pale uliponitoa

    Ningelikuwa natazama ya binadamu
    (hakika leo) fadhila yake ingelikuwa madharau
    Lakini wewe utoaye hewa na maji
    (watugawia) tajiri hata walemavu na maskini

  2. Na marafiki, walinipenda wengi sana
    Nilipokuwa na gari na nyumba yenye kupendeza
    Walinipenda, pale pesa zilipoisha
    Majuto niliyapata, nilipoachwa peke yangu
  3. Maisha yangu, yalipokuwa yenye shida
    Hakika ulinitoa, nilipoanguka shimoni
    Baraka nyingi, ulimimina kwangu mimi
    Hata nao majirani, sasa wamebaki butwaa
  4. Ninashukuru, kwa kunikinga na ajali
    Ninaposafiri mimi, umekuwa dereva wangu
    Pia magonjwa, umeyapiga teke kwangu
    Hakika nina sababu, ya kutamka sifa zako