Upendo Kupita Upeo
Upendo Kupita Upeo | |
---|---|
Alt Title | Ee Mungu Wangu |
Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
Album | Ushuhuda Tosha |
Category | Thanksgiving / Shukrani |
Composer | J. C. Shomaly |
Views | 7,471 |
Upendo Kupita Upeo Lyrics
- Ee Mungu wangu, kwa hakika unanipenda
Upeo wa macho yangu, sijui nikulipe nini
Maisha yangu, nayatazama nashukuru
Kwa yote uliyotenda, na pale uliponitoaNingelikuwa natazama ya binadamu
(hakika leo) fadhila yake ingelikuwa madharau
Lakini wewe utoaye hewa na maji
(watugawia) tajiri hata walemavu na maskini - Na marafiki, walinipenda wengi sana
Nilipokuwa na gari na nyumba yenye kupendeza
Walinipenda, pale pesa zilipoisha
Majuto niliyapata, nilipoachwa peke yangu - Maisha yangu, yalipokuwa yenye shida
Hakika ulinitoa, nilipoanguka shimoni
Baraka nyingi, ulimimina kwangu mimi
Hata nao majirani, sasa wamebaki butwaa - Ninashukuru, kwa kunikinga na ajali
Ninaposafiri mimi, umekuwa dereva wangu
Pia magonjwa, umeyapiga teke kwangu
Hakika nina sababu, ya kutamka sifa zako