Namtegemea Mungu
Namtegemea Mungu | |
---|---|
Performed by | St. Augustine University of Dsm |
Album | Namtegemea Mungu |
Category | Thanksgiving / Shukrani |
Composer | Erastus F. Jissu |
Views | 5,800 |
Namtegemea Mungu Lyrics
- { [ s ] Namtegemea Mungu, (aee Mungu)
Mimi namtegemea Mungu mimi } *2
Mimi namtegemea Mungu mimi
Mimi namtegemea Mungu mimi
{ Iyele iyele iyele iyele iyele!
Umeniumba vilivyo mimi leo nakutegemea
Hakika nimesema wewe Mungu nakutemea (aee) } *2
Katika maisha yangu nakutegemea wewe
Hata familia yangu yakutegemea wewe (ee Mungu)
Hivyo usiniache pekee wewe ni Mungu wangu
{ Hauna ubaguzi, umejaa huruma,
Wanadamu sote watupenda, hakika wewe ni mkuu } *2 - [ t ] Awali nikushukuru kwa kuniumba mimi,
Umeniumba tena kwa mfano wako
Niseme nini? niseme nini?
Niseme nini juu ya upendo wako
Ninakusifu, nakutukuza,
Nakuinua mbele ya miungu yote
{ Hakuna kama wewe, hakuna!
Hakuna kama wewe Mungu muumba wetu } *2 - [ t/b ] Muoneni baba, muoneni mama,
Muoneni kaka, muoneni dada
Walivyoumbwa na Mungu wetu, wote wapendeza
[ s/a ] Shangilia kwa makofi, Shangilia kwa makofi
Shangilia kwa makofi, huo ni utukufu wake - [ s/a ] Maisha yetu tumkabidhi Mungu, ayaongoze kila wakati
Tusijisifu tunapofanikiwa, mafanikio yatoka kwake
Usiisifu akili yako ndugu msifu Mungu wako - [ t/b ] Sitamwacha (haa) Mungu wangu (haa),
Siku zote (haa) anitunza (haa)
Si mwepesi (haa) wa hasira (haa),
Ni mwingi (haa) wa rehema (haa)
Tumwinue Mungu(haa), tumwinue leo(haa),
Tumwinue Mungu(haa), tumwinue leo(haa)
Iyolelelele (haa) iyolelelele (huu),
Tumwinue wapendwa tumwinue Mungu wetu
Hakika sitokuacha milele sitokuacha Mungu
Also recordedby St. Cecilia Tabora