Login | Register

Sauti za Kuimba

Namtegemea Mungu Lyrics

NAMTEGEMEA MUNGU

@ Erastus F. Jissu

 1. { [ s ] Namtegemea Mungu, (aee Mungu)
  Mimi namtegemea Mungu mimi } *2
  Mimi namtegemea Mungu mimi
  Mimi namtegemea Mungu mimi

  { Iyele iyele iyele iyele iyele!
  Umeniumba vilivyo mimi leo nakutegemea
  Hakika nimesema wewe Mungu nakutemea (aee) } *2

  Katika maisha yangu nakutegemea wewe
  Hata familia yangu yakutegemea wewe (ee Mungu)
  Hivyo usiniache pekee wewe ni Mungu wangu

  { Hauna ubaguzi, umejaa huruma,
  Wanadamu sote watupenda, hakika wewe ni mkuu } *2
 2. [ t ] Awali nikushukuru kwa kuniumba mimi,
  Umeniumba tena kwa mfano wako
  Niseme nini? niseme nini?
  Niseme nini juu ya upendo wako
  Ninakusifu, nakutukuza,
  Nakuinua mbele ya miungu yote
  { Hakuna kama wewe, hakuna!
  Hakuna kama wewe Mungu muumba wetu } *2
 3. [ t/b ] Muoneni baba, muoneni mama,
  Muoneni kaka, muoneni dada
  Walivyoumbwa na Mungu wetu, wote wapendeza
  [ s/a ] Shangilia kwa makofi, Shangilia kwa makofi
  Shangilia kwa makofi, huo ni utukufu wake
 4. [ s/a ] Maisha yetu tumkabidhi Mungu, ayaongoze kila wakati
  Tusijisifu tunapofanikiwa, mafanikio yatoka kwake
  Usiisifu akili yako ndugu msifu Mungu wako
 5. [ t/b ] Sitamwacha (haa) Mungu wangu (haa),
  Siku zote (haa) anitunza (haa)
  Si mwepesi (haa) wa hasira (haa),
  Ni mwingi (haa) wa rehema (haa)
  Tumwinue Mungu(haa), tumwinue leo(haa),
  Tumwinue Mungu(haa), tumwinue leo(haa)
  Iyolelelele (haa) iyolelelele (huu),
  Tumwinue wapendwa tumwinue Mungu wetu
  Hakika sitokuacha milele sitokuacha Mungu
Namtegemea Mungu
COMPOSERErastus F. Jissu
CHOIRSt. Augustine University of Dsm
ALBUMNamtegemea Mungu
CATEGORYThanksgiving / Shukrani
MUSIC KEYF Major
TIME SIGNATURE6
16
NOTES Open PDF


Also recordedby St. Cecilia Tabora
 • Comments