Ulimi ni Uovu

Ulimi ni Uovu
Performed bySt. Don Bosco Mirerani
AlbumRamani ya Mbinguni
CategoryTafakari
ComposerO. Okwako
Views5,411

Ulimi ni Uovu Lyrics

  1. Ni nani awezaye kuufuga ulimi, ulimi, ulimi *2
    Ulimi ni uovu huu, ulimi unaleta ugombanishi
    { Ulimi ulimi ulimi, ulimi ulimi ulimi
    Ulimi ulimi ulimi, ulimi kiungo kidogo
    Lakini una sumu kali iletayo mauti } * 2

  2. Ulimi ni kitu kiovu wala hakiwezi kutawalika
    Lakini kimejaa uovu, uovu uletao mauti
  3. Tazama tunamshukuru Muumba kwa kutumia ulimi
    Na tena twatumia ulimi huo kuwalaani wenzetu
  4. Tazama wote tumeumbwa kwa mfano na sura ya Mungu
    Maneno ya laana kusifu yatoka kweli kinywa kimoja

    //hitimisho//

    Je chemichemi moja yaweza kutoa maji matamu
    Je mti wa mpini waweza kuzaa zeituni
    Wala chemichemi ya maji ya chumvi kutoa maji matamu
    Je chemichemi moja yaweza kutoa maji machungu
    Je mti wa zabibu waweza zaa tunda la mpini
    Wala chemichemi ya maji ya chumvi kutoa maji matamu