Zimetiririka
| Zimetiririka | |
|---|---|
| Alt Title | Neema za Mungu | 
| Performed by | St. Maria de Martha - Mbezi Beach | 
| Album | Zimetiririka | 
| Category | Thanksgiving / Shukrani | 
| Composer | Victor Aloyce Murishiwa | 
| Views | 17,615 | 
Zimetiririka Lyrics
- Zimetiririka zimetiririka,
 Zimetiririka neema za Mungu{ Zimetiririka, neema zimetiririka, neema zimetiririka
 Wote tumeinuliwa aleluya } *2
 { Majumbani mwetu (zimetiririka)
 Mashambani mwetu (zimetiririka tiririka)
 Familia zetu (zimetiririka) tumeinuliwa aleluya } *2
- Tazama mimea inavyochanua,
 Hizi ni neema kutoka Mbinguni
- Tazama bahari na mawimbi yake
 Vinashangilia neema za Mungu
- Tazama wanyama wanavyopendeza
 Ndege wa angani wanaburudisha
- Mvua inanyesha jua inawaka
 Kuukamilisha utukufu wake
- Mchana na usiku vinatuongoza
 Kuyafurahia majira ya mwaka
- Mbingu zafurahi na mawingu yote
 Vinashangilia neema za Mungu
 
  
         
                            