Shukrani ya Mwili
   
    
     
         
          
            Shukrani ya Mwili Lyrics
 
             
            
- Nimeunakishi mwili wangu kwa marashi na kwa saluni
 Na nimeulisha chakula safi na ukashiba
 Nimehangaika kuupamba - kwa mavazi ya kupendeza
 Na nikaunywesha kila kinywaji ukaburudika
 Tazama shukrani ya mwili huu ni uchovu na ugonjwa
 Shukrani ya mwili kwangu ni usingizi
 Shukrani ya mwili huu ni kutorithika kamwe
 Shukrani ya mwili kwangu ni kurudi mavumbini, milele
 Milele milele hazina yangu mbinguni (kweli) *4
 Nimeuhifadhi kwenye nyumba ya kifahari na geti kubwa
 Na nikaajiri mlinzi bora wa kulinda nchi
 Nimeuhifadhi kwa mashuka chandarua na makapeti
 Na nikaulaza kwenye gondoro yenye raha tupu
- Nimeushibisha kwa anasa na starehe za kila namna
 Na hata zile zinazotumia mwili wa wengine
 Nimeukusanyia kiburi cha ujanja na ujuaji
 Na nikaupatia utukufu machoni pa watu