Shukrani ya Mwili

Shukrani ya Mwili
ChoirSt. Don Bosco Mirerani
AlbumRamani ya Mbinguni
CategoryTafakari
ComposerBernard Mukasa

Shukrani ya Mwili Lyrics

 • Nimeunakishi mwili wangu kwa marashi na kwa saluni
  Na nimeulisha chakula safi na ukashiba
  Nimehangaika kuupamba - kwa mavazi ya kupendeza
  Na nikaunywesha kila kinywaji ukaburudika

  Tazama shukrani ya mwili huu ni uchovu na ugonjwa
  Shukrani ya mwili kwangu ni usingizi
  Shukrani ya mwili huu ni kutorithika kamwe
  Shukrani ya mwili kwangu ni kurudi mavumbini, milele
  Milele milele hazina yangu mbinguni (kweli) *4

  Nimeuhifadhi kwenye nyumba ya kifahari na geti kubwa
  Na nikaajiri mlinzi bora wa kulinda nchi
  Nimeuhifadhi kwa mashuka chandarua na makapeti
  Na nikaulaza kwenye gondoro yenye raha tupu
 • Nimeushibisha kwa anasa na starehe za kila namna
  Na hata zile zinazotumia mwili wa wengine
  Nimeukusanyia kiburi cha ujanja na ujuaji
  Na nikaupatia utukufu machoni pa watu