Imani Yangu
Imani Yangu | |
---|---|
Performed by | St. Maria Goretti Karatu Dar-es-Salaam |
Album | Tazama Safina |
Category | Faith |
Composer | Victor Aloyce Murishiwa |
Views | 11,701 |
Imani Yangu Lyrics
Nipo katikati ya Mbingu na ardhi, ninaning'inia sina pa kushika
Duniani sipo na mbinguni sipo, ninawayawaya Bwana niokoe
/s/
Nikienda huku, mambo motomoto, nikirudi kule, ni baridi tupu
Mbele yangu giza, nyuma yangu giza, mahubiri mengi yananiyumbisha imani
/a/
Kumtafuta Mwokozi, ee Mungu uko wapi ili nije kwako hima,
Mbele yangu kuna giza nene na nyuma yangu ni giza
Mahubiri mengi yamezidi na mengine yananiyumbisha imani, imani
/t/
Nikienda huku ninabatizwa, lakini nikirudi kule ninaitwa mimi kafiri
Giza pande zote, mahubiri ni mengi, na mengine yananiyumbisha imani imani
/b/
Nikienda huku ni moto, nikirudi huku baridi, vuguvugu haitakiwi
Na imani yangu yayumba Mungu wangu nisaidie niokoe nisipotee
mahubiri mengi na mengine yananiyumbisha imani- Roho yangu Bwana inakutamani,
wewe peke yako ndiwe tiba yangu
neno lako Bwana litaniponya
Rudi Bwana Yesu njoo kwetu hima
Ulimwengu huu, ulioufia
Umekuwa jela ya maskini - Manabii wengi wananiyumbisha
Nimfuate yupi, nimuache yupi
Wapo wa uongo, wapo wa kwei
Kwa sababu wewe, Mungu ni mmoja
Twakuomba Baba utuunganishe
Matabaka yote na yatoweke