Majibu ya Msalaba
   
    
     
         
          
            Majibu ya Msalaba Lyrics
 
             
            
- Nimejua waziwazi yanapotoka haya,
 Na ninayoyatafuta usiku mchana
 Yanatoka kwa kiasi na kiwango kamili
 Kwa wakati ufaao na lugha sahihi
 Yamepita kimo changu cha kuyatafakari
 Yana raha mwisho wake machungu mwanzoni
 { Yaone, hayakujificha, kabisa, yamefunuliwa
 Kwa yule, aliyefunuka, aliye, moyo wazi ae }*2
 Nimeyaona, nimeyatambua!
 { Majibu majibu he!
 Yanatoka pale kwenye msalaba juu }* 2
 { Kimbilio-
 ah ah aeeh msalaba huu wa Yesu
 Tumaini-
 ah ah aeeh msalaba huu wa Yesu } *2
- Kujua kujizuia yale yenye unono
 Kujua kuyapokea yale machungu chungu
- Kukubali kupokea hasara bila kosa
 Kusudi kumsamehe yule aliyekosa
- Kukabidhi maumivu kwa Yesu bila shaka
 Na kuacha kupanga majibu na muda wake
- Kuamini bila mwisho ingawa sijaona
 Kutumaini ya kwamba Yesu aweza yote