Majibu ya Msalaba

Majibu ya Msalaba
Performed byMoyo Safi (Unga Ltd)
AlbumMilele Milele Nitakusifu
CategoryTafakari
ComposerBernard Mukasa
Views4,987

Majibu ya Msalaba Lyrics

  1. Nimejua waziwazi yanapotoka haya,
    Na ninayoyatafuta usiku mchana
    Yanatoka kwa kiasi na kiwango kamili
    Kwa wakati ufaao na lugha sahihi
    Yamepita kimo changu cha kuyatafakari
    Yana raha mwisho wake machungu mwanzoni
    { Yaone, hayakujificha, kabisa, yamefunuliwa
    Kwa yule, aliyefunuka, aliye, moyo wazi ae }*2
    Nimeyaona, nimeyatambua!

    { Majibu majibu he!
    Yanatoka pale kwenye msalaba juu }* 2
    { Kimbilio-
    ah ah aeeh msalaba huu wa Yesu
    Tumaini-
    ah ah aeeh msalaba huu wa Yesu } *2

  2. Kujua kujizuia yale yenye unono
    Kujua kuyapokea yale machungu chungu
  3. Kukubali kupokea hasara bila kosa
    Kusudi kumsamehe yule aliyekosa
  4. Kukabidhi maumivu kwa Yesu bila shaka
    Na kuacha kupanga majibu na muda wake
  5. Kuamini bila mwisho ingawa sijaona
    Kutumaini ya kwamba Yesu aweza yote