Mambo ya Yesu
Mambo ya Yesu Lyrics
{ Hatutaacha kuyanena mambo ya Yesu
Hatutaacha kuyasimulia matendo yake Kristu } *2
(Sisi) uliyoyaona na kuyasikia wenyewe (Yesu)
Akimwaga damu yake msalabani tukombolewe
Tuliyoyaona na kuyasikia wenyewe (hivyo)
Maisha yangu na uhai wangu mimi namkabidhi Yesu
- Amewaponya wenye magonjwa wakawa huru
Akawafufua wafu nao wakawa hai
Ni nani kama Yesu na hakuna aliye kama Yesu
- Alitoa uhai wake kwa ajili yetu
Akafa kifo cha aibu pale msalabani
Ni nani kama Yesu na hakuna aliye kama Yesu
- Ametuachia karamu iliyo kuu,
Karamu ya upatanisho nay a upendo
Ni nani kama Yesu na hakuna aliye kama Yesu
- Alibadilisha maji yakawa divai
Na wenye harusi wakanywa wakafurahi
Ni nani kama Yesu na hakuna aliye kama Yesu